logo image

TYD YATOA FURSA KWA WABUNIFU (TYD PROVIDES OPPORTUNITY FOR INNOVATORS)



Tyd Innovation Incubator

"TYD Innovation Incubator ikiwa kama mdau anayependa kuchagiza maendeleo endelevu ya viwanda nchini Tanzania kupitia ubunifu na wabunifu wa ndani ya Tanzania na Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania, imeonelea kuwa sasa ni muda muafaka wa kukaribisha mtu yeyote na zaidi ni kijana, ambaye ana wazo la kiubunifu". Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Incubator hiyo Bwana Geofrey Chami, siku ya Jumanne tarehe 17 Aprili, 2018 wakati anatoa taarifa kukaribisha wabunifu wapya.

Imeelezwa kuwa, TYD inatambua changamoto ambazo jamii yetu inakumbana nazo, na pia inatambua changamoto ambazo wabunifu wa kitanzania wanakumbana nazo wanapohitaji kurasimisha ubunifu wao kuwa jawabu la matatizo ya jamii zetu. Na ndiyo maana ikaanzisha mfumo wa kupokea mawazo ya kiubunifu na majawabu yake kisha yenyewe kuwa sehemu ya kurasimisha majawabu hayo kwa ajili ya kusaidia jamii ya kitanzania, tena katika kipindi hiki ambacho sera kubwa ya Taifa ni ukuaji wa uchumi wa viwanda.

TYD ambayo ilianza rasmi mwaka jana (2017) kwa Rasilimali ndogo sana za Watanzania wenye nia ya kusimamia ubunifu bila ya kutegemea pesa za wahisani au wawekezaji, mpaka sasa imefanikiwa kukamilisha miradi midogo miwili ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), na iko mbioni kukamilisha miradi mingine miwili, kisha itaanza utekelezaji wa miradi yake mikubwa ambayo imo kwenye mipango ya muda mrefu. Hayo yote yalifanyika kwa ajili ya kuifanya “Incubator” hiyo iwe na kitu cha kuonesha kabla ya kukaribisha wawekezaji au wafadhili ambao tayari wameshaanza kuonesha nia ya kuongeza nguvu, lakini pia kuiwezesha kuingiza kipato cha kujiendesha.

Hivyo TYD imewakaribisha watu wote wanaohisi kuwa ni wabunifu, kwanza kwa kuwasilisha wazo la kiubunifu, kujiunga na taasisi na kisha kutengeneza jawabu la wazo hilo kwa kushirikiana na wataalamu wengine waliopo tayari.

Vilevile, endapo wazo husika litahitaji uwekezaji wa kifedha zaidi, TYD itawavutia wawekezaji na wafadhili na hivyo kugeuza wazo husika kuwa biashara ambayo mleta wazo atanufaika nalo katika kipindi chote ambacho wazo husika litakuwa likitumika kama jawabu la kutatua changamoto fulani kwenye jamii yetu.

Bonyeza hapa kutuma wazo lako

“TYD Innovation Incubator as one of the stakeholders fostering Industrial sustainable development in Tanzania through Innovation and Innovators who are in Tanzania and Tanzanian Diasporas, finds it the right time to invite everyone especially youth with any innovative idea”. That has been said by its Managing Director Mr. Geofrey Chami on Tuesday 17th April, 2018 when making a public declaration on inviting new Innovators.

It is stated that TYD recognizes the challenges our society faces, and also recognizes challenges that Tanzanian Innovators face when they need to consolidate their creativity as an answer to the problems that our society faces. And that is why it has developed a system for receiving innovative ideas and its solutions, and standing as a part of consolidating those solutions for supporting the Tanzanian community, taking into consideration that the mostly implemented national policy currently is the growth of Industrial Economy.

TYD was established in 2017 with very minimum resources from Tanzanians who believed in nurturing in innovation without support from any donor and/or investor. Recently it has commissioned two small quick-win projects on Information and Communication Technology (ICT) and two more are underway before initiation of long term bigger projects. While the main aim of implementing quick-win projects was to ensure that the Incubator gain some income for its daily operation, they were also designed to attract Investors and/or Donors who have already started showing interest.

So the TYD has welcomed all who think they are creative, first by presenting an innovative idea, joining the institution and then developing a solution of the submitted idea in collaboration with other existing experts.

Similarly, if the idea will require more financial investments, the TYD will attract investors and donors and thus convert the relevant idea into a business that the Innovator will benefit from throughout the period that the relevant idea will be used as a solution to solving some challenges in our society.

Click here to submit your Innovative Idea